Ikiwa tamaduni za muafrika zinawataka watu wavae
nguo za staha na heshima, huko Kenya wanawake na baadhi ya wanaume wameandamana
wakishinikiza kuwa wanawake wanauhuru wakuvalia mavazi wanayofurahishwa nayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke mmoja kuvuliwa
nguo na wanaume wiki iliyopita kwenye kituo cha magari cha abiria huko Nairobi
kisa amevaa nguo fupi. Waandamani wamepinga vikali kitendo hicho.
Baadhi ya wanaharakati, wasanii na watu maarufu
wamesema kwa hali hiyo basi hata wanaume wanaovalia mlegezo nao wavuliwe nguo.
Maandamano hayo yalienda sambamba na kauli mbiu ya "ma dress my choice"
Chanzo: BBC