Serikali ya Kenya imezindua mfumo wa kielektroniki
utakao iwezesha kugundua wafanyakazi bandia wa utimishi wa umma.
Akizindua shughuli za kung’amua wafanyakazi bandia jana raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema lengo sio kuwafukuzisha kazi wafanyakazi wa
umma bali nikuhakikisha wakenya wanapata huduma bora wanazo hitaji.
Shughuli hizo zina husisha mfumo wa kuchukua maelezo
ya watumishi wote wa umma kupitia njia ya kusajili majina ya wafanyakazi wote
kwa njia ya kielektroniki.
Raisi Kenyatta amewataka wafanyakazi wote kushiriki
katiza zoezi hilo la usajili ili kukamilisha zoezi hilo kwa muda uliopangwa ili
waweze kudhibiti tatizo hilo la wafanyakazi bandia ambalo limekuwa kikwazo kwa serikali.
Chanzo.Irib Swahili
0 comments:
Post a Comment