Hoja binafsi
Inchini Tanzania
ugonjwa wa ukimwi umeingia tangu miaka ya 80. Tangu kipindi hicho mpaka hivi
sasa serekali pamoja na mashirika mbali mbali ya watu binafsi na pamoja na
mashirika ya kimataifa yamekuwa yakijikita kwenye harakati za kuzuia maambukizi
ya ugonjwa wa ukimwi.
Elimu juu ya ugonjwa
huu sugu imekuwa ikitolewa kwa makundi yote ya jamii yani kuanzia watu wazima,
vijana pamoja na watoto. Mkazo zaidi umekuwa ukitolewa kwa vijana pamoja na
watoto kwani makundi hayo ndio yapo hatarini zaidi kupata maambukizi.
Ikiwa ni sikuchache tu
zilizopita Afrika imeazimisha siku ya mtoto wa Afrika, leo tuta angalia wajibu
wa wazazi kuwaanda watoto ili waweze
kupambana na vita dhidi ya tabia hatarishi, ambazo zinaweze kupelekea watoto kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi pamoja na magonjwa mengine
ya zinaa.
Wazazi wengi baada ya
kuwapeleka watoto wao shule hufikiri wamemaliza kazi yao ya malezi na kuwaachia
walimu mzigo wote wa kuwaandaa watoto kupambana na changa moto mbali mbali
zinazo wa kabili hususani ni vita dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Wazazi wamekuwa wazito
pengine ni kutokana na kutingwa na kazi au wengine ni kutotilia maanani swala
la malezi na baadhi yao ulevi wa kupindukia unao sababisha wao kuchelewa kurudi
nyumbani na kukuta watoto wao wame lala.
Dunia ya leo
inachangamoto kubwa sana kwani utandawazi umekuwa ukiwafanya vijana na pengine
ata wazee kusahau maadili mema ya kwao na kujikuta wakijiingiza kwenye mambo
yasio na manufaa kwao. je watoto wasipo pewa malezi bora wataweza kuishi kwa
maadili mema?
Wazazi inawapasa wawe
makini na kufuatilia mienendo wa watoto wao. Inabidi wazazi wajijengee
utaratibu wa kuwaweka chini watoto wao na kuvunja ukimwa na kutilia mkazo yale
watoto wanayo fundishwa shuleni hususani elmu juu ya UKIMWI.
mfano jinsi ya kuepukana na tabia hatarishi kama kuvuta bangi, sigara, kunywa pombe,kuangalia filamu za ngono na kujihusisha na vitendo vya zinaa kama walimu wao wanavyo wafundisha wakiwa mashuleni.
mfano jinsi ya kuepukana na tabia hatarishi kama kuvuta bangi, sigara, kunywa pombe,kuangalia filamu za ngono na kujihusisha na vitendo vya zinaa kama walimu wao wanavyo wafundisha wakiwa mashuleni.
Ukali wa wazazi kwa
watoto haujengi bali unatengeneza uadui bainia yao na inakuwa vigumu watoto wao
kuwa wazi mbele yao na kuwaeleza mambo tofauti tofauti wanayo kutana nayo mitaani
au mshuleni. Wazazi wakitengeneza
utamaduni mzuri wa urafiki na watoto wao, itawasidia kujua mienendo ya watoto
wao na kujua wapi pakurekebisha na kutilia mkazo ili kuhakikisha watoto wao
wanakuwa salama wakati wote.
Watoto hupendelea
kuangalia tv, na baadhi yao hupendelea kuingia kwenye mitandao hasa watoto wa mjini. Hupendelea kangalia mambo
mbali mbali kama kuangalia miziki, filamu
pamoja na picha za wasanii na mambo mengine.
Ingawaje nyumbani wazazi wana weza kuhakikisha
watoto wana angalia au kutafuta mambo yanayo wafaa kwenye mitandao lakini huduma
iyo hutolewa mitaani kwa malipo kiasi na
baadhi ya watoto hutumia mwanya huo kuangalia
mambo yasiyo faa mfano picha za utupu.
Ukiachana na ilo, kuna
majumba ya sinema ambayo huonesha filamu za ngono na watoto wakiwepo bila
kujali ili mradi wamelipia kiingilio. Tabia hizi ni hatarishi na zina weza
kuwashawishi watoto kujihusisha na zinaa na watoto wenzao au hata watu wazima.
Hivyo basi wanatengeneza nafasi ya wao kupata
maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kuna vipindi vizuri
sana kwenye tv vinavyo wafaa watoto. vipndi vya burudisha kama vile michezo katuni na vingine
vya kuwaelimisha kwa kutanua uelewa wao juu ya maswala mbali mbali katika jamii
ikiwemo pia vipindi vinvavyo toa elimu juu ya ugonjwa wa ukimwi.
Wazazi ndio wenye
jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wao wanaangalia
vipindi vinavyo wafaa pia matumizi mazuri ya mitandao mda wote. Mfanya kazi wa
ndani sio rahisi kumsimamia mototo kwenye jambo hili kutokana na kuwa na
shunguli nyingi za kufanya na wengine kuwa na uelewa mdogo kwani baadhi yao unaweza
ukawakuta wana tazama picha zisizo faa wakiwa pamoja na watoto bila kujali.
Pia kwa upande mwingine
wazazi wana paswa kuwajengea watoto wao msingi mzuri wa imani wakiwa bado
wadogo ili iwasaidie waweze kuishi katika msingi huo mpaka watakapo kuwa wakubwa
na hivyo basi kuepukana na tabia zinazo kinzana na mafundisho ya dini zao kama
vile kuzini kabla ya ndoa au nnje ya ndoa.
Pengine inawawia vigumu
baadhi ya wazazi kuwasimamia watoto wao kwenda kwenye mafundisho ya dini kutokana
na kwanza wao wenyewe sio waudhuriaji wazuri wa ibada na shughuli mbali mbali
za kidini.
Kiujumla mapambano dhidi
ya ugonjwa wa ukimwi kwa watoto ni jukumu la jamii nzima. Watoto wenyewe, wazazi pamoja na walimu. Ushirikiano wao
ndio utawezesha kuwasaidia watoto kujiandaa na mupambano dhidi ya changamoto
mbali mbali zinazo wakabili watoto hususani
utandawazi.
Wahenga walisema “samaki mkunje angali
mbichi” nivigumu sana
kumbalilisha mtu tabia akiwa amesha kuwa mtu mzima ndo maana elimu ya ukimwi
inatolewa sana kwa vijana pamoja na watu wazima lakini maambukizi yamekuwa
yakiongezeka sana hasa kwa watu walio kwenye ndoa.
Kwa hali hiyo basi
wazazi kushirikiana na walimu wana jukumu kubwa sana kuhakikisha wana waandaa
watoto vizuri ili waweze kuepukana na tabia hatarishi zinazo weza kuwapelekea
watoto wao kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Arnold musaroche
Tumaini University
0718636856
0 comments:
Post a Comment