Kaimu Meneja Magari kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) Bw. Julius Mchihiyo (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa
mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Mradi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Bw. Ramadhani Sengali akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua
jinsi gani mfumo huo utaleta tija hasa katika ukususanyaji wa kodi, kwenye
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari, kulia
ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka hiyo Bw. Richard
Kayombo.
{PICHA ZOTE NA HASSAN
SILAYO}
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Imeeleza kuwa Kuanzia mwezi Agosti 2013 malipo
yote ya ada za mwaka za magari (annual road license) yatafanywa kwa njia ya mtandao
kwa maana ya kutumia simu za kiganjani, benki na wakala wa Maxmalipo.
Hii inatokana na maboresho
ya mifumo ya kielektroniki ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kuyafanya
ikiwa ni juhudi za kutoa huduma bora kwa walipakodi na kuhakikisha kuwa mapato
ya Serikali yanayokusanywa na yanawasilishwa kwa wakati kwenye mfuko mkuu wa
Serikali, Benki Kuu.
Mfumo huu utatumika kulipa
ada za mwaka za magari ambapo mlipakodi anaweza kupata taarifa ya kiasi cha
kodi anachotakiwa kulipa.
Utaratibu wa kutumia mtandao kulipa ada za magari:
- Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za gari mfano KADIRIA T171AUC kwenda namba 15341.
- Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
- Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, MPESA, AIRTELMONEY au wakala wa MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.
0 comments:
Post a Comment