Published with Blogger-droid v2.0.10
Friday, November 15, 2013
Tuesday, July 30, 2013
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF) WAZINDUA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI
Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bi.Constantina Martin (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Mpango Mpya wa
uchangiaji wa hiari mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi wasio wanachama wa
mifuko ya hifadhi ya jamii fursa ya kujiunga na mfuko huo, kushoto ni
Mkurugenzi wa Uwekezaji, mipango na Utafiti Bw. Gabriel Silayo.
Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mipango na Utafiti kutoka
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Gabriel Silayo (kushoto)
akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo yaliyofikiwa na mfuko huo tangu kuanzishwa
kwake kulia ni Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko huo
Bi.Constantina Martin.
PICHA
NA FRANK MVUNGI
Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi kutoka (PSPF) Bi.Constantina Martin amesema Mpango huu wa hiari ni mahsusi kwa ajili ya kuwapatia
huduma ya hifadhi ya jamii wale wote ambao awali kutokana na matakwa ya
kisheria hawakuweza kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Vile vile mpango huu ni fursa nzuri ya kujiwekea
akiba ya ziada wanachama ambao tayari wamo katika Mifuko mbalimbali ya Hifadhi
ya Jamii.
Ameongeza kuwa, uanachama katika mpango huu uko wazi kwa kila Mtanzania
mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Kiasi cha mchango kwa mwezi ni shilingi 10,000/= kiwango ambacho wengi
wanaweza kukimudu kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu. Michango inaweza
kuwasilishwa kwa siku, wiki, mwezi na hata kwa msimu kutegemeana na upatikanaji
wa kipato cha ziada. Michango hii huwekewa faida kila baada ya miezi sita.
Michango inaweza kuwasilishwa kupitia akaunti ya benki,
au kupitia Wakala wa malipo wa M-Pesa, Tigo-Pesa na Airtel money. Mwanachama
atajaza fomu na kupewa kitambulisho na nambari ya uanachama.
Mafao yatolewayo katika mpango huu wa hiari ni kama Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali, Fao la Uzeeni,Fao la Ugonjwa na Fao la Kifo.
Pia mwanachama anapolazimika kuchukua michango yake yote
na faida kutokana na sababu zozote zile, anaweza tena kuanza kuchangia upya
bila masharti yoyote.
Monday, July 29, 2013
MFUMO MPYA WA KULIPA ADA ZA MWAKA ZA MAGARI KWA NJIA YA MTANDAO
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Richard Kayombo (kulia) akieleza kwa
waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya
mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara
ya Habari kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mamlaka hiyo Bw. Ramadhani Sengali.
Utaratibu wa kutumia mtandao kulipa ada za magari:
Kaimu Meneja Magari kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) Bw. Julius Mchihiyo (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa
mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Mradi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Bw. Ramadhani Sengali akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua
jinsi gani mfumo huo utaleta tija hasa katika ukususanyaji wa kodi, kwenye
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari, kulia
ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka hiyo Bw. Richard
Kayombo.
{PICHA ZOTE NA HASSAN
SILAYO}
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Imeeleza kuwa Kuanzia mwezi Agosti 2013 malipo
yote ya ada za mwaka za magari (annual road license) yatafanywa kwa njia ya mtandao
kwa maana ya kutumia simu za kiganjani, benki na wakala wa Maxmalipo.
Hii inatokana na maboresho
ya mifumo ya kielektroniki ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kuyafanya
ikiwa ni juhudi za kutoa huduma bora kwa walipakodi na kuhakikisha kuwa mapato
ya Serikali yanayokusanywa na yanawasilishwa kwa wakati kwenye mfuko mkuu wa
Serikali, Benki Kuu.
Mfumo huu utatumika kulipa
ada za mwaka za magari ambapo mlipakodi anaweza kupata taarifa ya kiasi cha
kodi anachotakiwa kulipa.
Utaratibu wa kutumia mtandao kulipa ada za magari:
- Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za gari mfano KADIRIA T171AUC kwenda namba 15341.
- Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
- Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, MPESA, AIRTELMONEY au wakala wa MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.
Subscribe to:
Posts (Atom)



