Wizara ya viwanda na biashara imewataka wafanya biashara
inchini kutumia vyema fursa walizo nazo kwa kufanya biashara na nchi wahisana
wa Afrika mashariki, kwani wao kama wizara wamejitaidi kujenga mahusiano mazuri
na inchi za ukanda huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
mapema leo hafisa habari na mawasiliano wa wizara hiyo Bw. Nikodemas Mushi
amewataka wafanya biashara wafike wizarani ili wapata maelekezo jinsi gani
wanaweza kufanya biashara kwenye soko la Afrika mashariki, pamoja na SADEC.
“wafanya biashara wanapaswa kuuza vitu vyenye ubora unao hitajika pamoja na ujazo stahiki ili waweze
kupata soko kwenye jumuiya ya Afrika mashariki, hivyo basi ningezitaka kampuni
na taasisi kuwekeza katika utengenezaji wa vifungashio ili kuwasidia wajasiria mali wadogo wadogo
kuepukana na kutumia vifungashio visivyo na ubora” alisema
Mushi pia aliwata wafanya biashara kuzingatia ujazo ulio
sahihi nakuacha kujaza lumbesa.
Hata ivyo hafisa huyo wa habari amesema pamoja na kufanya
operesheni mbali mbali za kushtukiza ili kubaini bidhaa ambazo hazija thibitiswa
na mamlaka ya viwango (TBS) amewataka pia wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo ili
kubaini bidhaa zinazo ingizwa inchini kinyemela kwani nyingi zinakua hazina
ubora.
Arnold Musaroche
0656 606095
0 comments:
Post a Comment