Pages

Labels

Monday, November 17, 2014

WAANDAMANA KUPINGA VITENDO VYA WANAWAKE KUVULIWA NGUO:KENYA


Ikiwa tamaduni za muafrika zinawataka watu wavae nguo za staha na heshima, huko Kenya wanawake na baadhi ya wanaume wameandamana wakishinikiza kuwa wanawake wanauhuru wakuvalia mavazi wanayofurahishwa nayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke mmoja kuvuliwa nguo na wanaume wiki iliyopita kwenye kituo cha magari cha abiria huko Nairobi kisa amevaa nguo fupi. Waandamani wamepinga vikali kitendo hicho.

Baadhi ya wanaharakati, wasanii na watu maarufu wamesema kwa hali hiyo basi hata wanaume wanaovalia mlegezo nao wavuliwe nguo.
Maandamano hayo yalienda sambamba na kauli mbiu ya "ma dress my choice"
Chanzo: BBC

Tuesday, September 2, 2014

KENYA KUWANASA WAFANYA KAZI BANDIA.



Serikali ya Kenya imezindua mfumo wa kielektroniki utakao iwezesha kugundua wafanyakazi bandia wa utimishi wa umma.

Akizindua shughuli za kung’amua wafanyakazi bandia jana raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema lengo sio kuwafukuzisha kazi wafanyakazi wa umma bali nikuhakikisha wakenya wanapata huduma bora wanazo hitaji.

Shughuli hizo zina husisha mfumo wa kuchukua maelezo ya watumishi wote wa umma kupitia njia ya kusajili majina ya wafanyakazi wote kwa njia ya kielektroniki.

Raisi Kenyatta amewataka wafanyakazi wote kushiriki katiza zoezi hilo la usajili ili kukamilisha zoezi hilo kwa muda uliopangwa ili waweze kudhibiti tatizo hilo la wafanyakazi bandia ambalo limekuwa kikwazo kwa serikali.
Chanzo.Irib Swahili

Sunday, August 3, 2014

381 WAFARIKI CHINA



Vifo zaidi vyazidi ongezeka kufwatia tetemeko la ardhi lililo ikumba jimbo la Yunnan Kusini magharibi mwa nchi ya China siku ya Jumapili alasiri

Watu 381 wameripotiwa kufariki kutokana na tetemeko hilo na maelfu ya watu walio dhurika wapo katika maeneo ambayo ni vigumu kufikika kutokana na uaribifu wa miundo mbinu aliotokea.

Vikosi vya uokoaji vinafanya kazi ya ziada kuhakikisha vinafikia maeneo yote yaliyo athirika lakini hofu zaidi ni mvua zinazo tarajiwa kunyesha ndani ya siku tatu zijazo zinazo weza kuwa kikwazo kwenye shughuli za uokoaji.
Chanzo: CCTV

Friday, December 20, 2013

Monday, December 9, 2013

Published with Blogger-droid v2.0.10

Siku ya Kimataifa ya kusherekea vyakula vya Asili (Terra Madre Day)

Baadhi ya vyakula vilivyo andaliwa na Chama cha wamama wastaafu wa eneo la Regent Estate Mikocheni jijiji Dar es Salaam wakati wakisherekea siku ya vyakula vya asili Duniani.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Siku ya Kimataifa ya kusherekea vyakula vya Asili (Terra Madre Day)

Baadhi ya vyakula vya asili vilivyo andaliwa na Chama cha kina mama wastaafu wanaoishi eneo la Regent Estate Mikocheni jijini Dar es Salaam

Published with Blogger-droid v2.0.10

Friday, November 15, 2013

Tuesday, July 30, 2013

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF) WAZINDUA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI

Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bi.Constantina Martin (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Mpango Mpya wa uchangiaji wa hiari mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi wasio wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii fursa ya kujiunga na mfuko huo, kushoto ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, mipango na Utafiti Bw. Gabriel Silayo.
Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mipango na Utafiti kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Gabriel Silayo (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo yaliyofikiwa na mfuko huo tangu kuanzishwa kwake kulia ni Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko huo Bi.Constantina Martin.
PICHA NA FRANK MVUNGI

Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi kutoka  (PSPF) Bi.Constantina Martin amesema Mpango huu wa hiari ni mahsusi kwa ajili ya kuwapatia huduma ya hifadhi ya jamii wale wote ambao awali kutokana na matakwa ya kisheria hawakuweza kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.  Vile vile mpango huu ni fursa nzuri ya kujiwekea akiba ya ziada wanachama ambao tayari wamo katika Mifuko mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii.
Ameongeza kuwa, uanachama katika mpango huu uko wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.  Kiasi cha mchango kwa mwezi ni shilingi 10,000/= kiwango ambacho wengi wanaweza kukimudu kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu. Michango inaweza kuwasilishwa kwa siku, wiki, mwezi na hata kwa msimu kutegemeana na upatikanaji wa kipato cha ziada. Michango hii huwekewa faida kila baada ya miezi sita.
Michango inaweza kuwasilishwa kupitia akaunti ya benki, au kupitia Wakala wa malipo wa M-Pesa, Tigo-Pesa na Airtel money. Mwanachama atajaza fomu na kupewa kitambulisho na nambari ya uanachama.
Mafao yatolewayo katika mpango huu wa hiari ni kama Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali,  Fao la Uzeeni,Fao la Ugonjwa na Fao la Kifo.
Pia mwanachama anapolazimika kuchukua michango yake yote na faida kutokana na sababu zozote zile, anaweza tena kuanza kuchangia upya bila masharti yoyote.

Monday, July 29, 2013

MFUMO MPYA WA KULIPA ADA ZA MWAKA ZA MAGARI KWA NJIA YA MTANDAO

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Richard Kayombo (kulia) akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mamlaka hiyo Bw. Ramadhani Sengali.


Kaimu Meneja Magari kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Julius Mchihiyo (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.



Meneja wa Mradi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Ramadhani Sengali akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua jinsi gani mfumo huo utaleta tija hasa katika ukususanyaji wa kodi, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari, kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka hiyo Bw. Richard Kayombo.
{PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO}

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Imeeleza kuwa Kuanzia mwezi Agosti 2013 malipo yote ya ada za mwaka za magari (annual road license) yatafanywa kwa njia ya mtandao kwa maana ya kutumia simu za kiganjani, benki na wakala wa Maxmalipo.
Hii inatokana na maboresho ya mifumo ya kielektroniki ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kuyafanya ikiwa ni juhudi za kutoa huduma bora kwa walipakodi na kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanayokusanywa na yanawasilishwa kwa wakati kwenye mfuko mkuu wa Serikali, Benki Kuu.

Mfumo huu utatumika kulipa ada za mwaka za magari ambapo mlipakodi anaweza kupata taarifa ya kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa.

Utaratibu wa kutumia mtandao kulipa ada za magari:

  1. Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za  gari mfano KADIRIA T171AUC kwenda namba 15341.  
  2. Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
  3. Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, MPESA, AIRTELMONEY au wakala wa MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.
Kuchukua cheti: (sticker ya gari): nenda katika ofisi yoyote ya TRA ukiwa na namba ya kumbukumbu uliyoitumia kufanya malipo