Pages

Labels

Tuesday, July 9, 2013

CHADEMA YA ITUPIA LAWAMA SEREKALIMwenyekiti  wa  chama  cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Bw. F. Mboye ameonesha hali ya masikitiko na kuitupia lawama serekali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa vitendo vinavyo fanywa na jeshi la polisi huko Mtwara.

Ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es salaam.

“Jeshi la polisi limeingia mtaani kwa lengo la kuleta hali ya amani lakini limeishia  kuwanyanyasa, kuwatesa, na kuwaonea wananchi wa mtwara na serekali imekaa kimya. “alisema.

Amevitaka vyombo vya dola vitimize wajibu wake wa kulinda amani na mali ya raia na siyo kuwatesa na kuwapiga wananchi kwa kuwasababishia vifo kinyume na haki za binadamu.

Kwa upande mwingine amevitupia lawama pia vyombo vya habari kwaku kaa kimya na kufumbia macho yale yanayo endelea huko Mtwara.

By Arnold Musaroche

0656606095 

1 comment: