Pages

Labels

Monday, November 17, 2014

WAANDAMANA KUPINGA VITENDO VYA WANAWAKE KUVULIWA NGUO:KENYA


Ikiwa tamaduni za muafrika zinawataka watu wavae nguo za staha na heshima, huko Kenya wanawake na baadhi ya wanaume wameandamana wakishinikiza kuwa wanawake wanauhuru wakuvalia mavazi wanayofurahishwa nayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke mmoja kuvuliwa nguo na wanaume wiki iliyopita kwenye kituo cha magari cha abiria huko Nairobi kisa amevaa nguo fupi. Waandamani wamepinga vikali kitendo hicho.

Baadhi ya wanaharakati, wasanii na watu maarufu wamesema kwa hali hiyo basi hata wanaume wanaovalia mlegezo nao wavuliwe nguo.
Maandamano hayo yalienda sambamba na kauli mbiu ya "ma dress my choice"
Chanzo: BBC

Tuesday, September 2, 2014

KENYA KUWANASA WAFANYA KAZI BANDIA.Serikali ya Kenya imezindua mfumo wa kielektroniki utakao iwezesha kugundua wafanyakazi bandia wa utimishi wa umma.

Akizindua shughuli za kung’amua wafanyakazi bandia jana raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema lengo sio kuwafukuzisha kazi wafanyakazi wa umma bali nikuhakikisha wakenya wanapata huduma bora wanazo hitaji.

Shughuli hizo zina husisha mfumo wa kuchukua maelezo ya watumishi wote wa umma kupitia njia ya kusajili majina ya wafanyakazi wote kwa njia ya kielektroniki.

Raisi Kenyatta amewataka wafanyakazi wote kushiriki katiza zoezi hilo la usajili ili kukamilisha zoezi hilo kwa muda uliopangwa ili waweze kudhibiti tatizo hilo la wafanyakazi bandia ambalo limekuwa kikwazo kwa serikali.
Chanzo.Irib Swahili

Sunday, August 3, 2014

381 WAFARIKI CHINAVifo zaidi vyazidi ongezeka kufwatia tetemeko la ardhi lililo ikumba jimbo la Yunnan Kusini magharibi mwa nchi ya China siku ya Jumapili alasiri

Watu 381 wameripotiwa kufariki kutokana na tetemeko hilo na maelfu ya watu walio dhurika wapo katika maeneo ambayo ni vigumu kufikika kutokana na uaribifu wa miundo mbinu aliotokea.

Vikosi vya uokoaji vinafanya kazi ya ziada kuhakikisha vinafikia maeneo yote yaliyo athirika lakini hofu zaidi ni mvua zinazo tarajiwa kunyesha ndani ya siku tatu zijazo zinazo weza kuwa kikwazo kwenye shughuli za uokoaji.
Chanzo: CCTV

Monday, December 9, 2013

Published with Blogger-droid v2.0.10

Siku ya Kimataifa ya kusherekea vyakula vya Asili (Terra Madre Day)

Baadhi ya vyakula vilivyo andaliwa na Chama cha wamama wastaafu wa eneo la Regent Estate Mikocheni jijiji Dar es Salaam wakati wakisherekea siku ya vyakula vya asili Duniani.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Siku ya Kimataifa ya kusherekea vyakula vya Asili (Terra Madre Day)

Baadhi ya vyakula vya asili vilivyo andaliwa na Chama cha kina mama wastaafu wanaoishi eneo la Regent Estate Mikocheni jijini Dar es Salaam

Published with Blogger-droid v2.0.10