Pages

Labels

Sunday, June 17, 2012

MTOTO WA AFRIKA NA MAPAMBANO ZIDI YA UKIMWI.







Hoja binafsi
Inchini Tanzania ugonjwa wa ukimwi umeingia tangu miaka ya 80. Tangu kipindi hicho mpaka hivi sasa serekali pamoja na mashirika mbali mbali ya watu binafsi na pamoja na mashirika ya kimataifa yamekuwa yakijikita kwenye harakati za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Elimu juu ya ugonjwa huu sugu imekuwa ikitolewa kwa makundi yote ya jamii yani kuanzia watu wazima, vijana pamoja na watoto. Mkazo zaidi umekuwa ukitolewa kwa vijana pamoja na watoto kwani makundi hayo ndio yapo hatarini zaidi kupata maambukizi. 
Ikiwa ni sikuchache tu zilizopita Afrika imeazimisha siku ya mtoto wa Afrika, leo tuta angalia wajibu wa wazazi kuwaanda watoto  ili waweze kupambana na vita dhidi ya tabia hatarishi, ambazo zinaweze kupelekea watoto  kupata maambukizi ya  ugonjwa wa ukimwi pamoja na magonjwa mengine ya zinaa.
Wazazi wengi baada ya kuwapeleka watoto wao shule hufikiri wamemaliza kazi yao ya malezi na kuwaachia walimu mzigo wote wa kuwaandaa watoto kupambana na changa moto mbali mbali zinazo wa kabili hususani ni vita dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. 
Wazazi wamekuwa wazito pengine ni kutokana na kutingwa na kazi au wengine ni kutotilia maanani swala la malezi na baadhi yao ulevi wa kupindukia unao sababisha wao kuchelewa kurudi nyumbani na kukuta watoto wao wame lala.
Dunia ya leo inachangamoto kubwa sana kwani utandawazi umekuwa ukiwafanya vijana na pengine ata wazee kusahau maadili mema ya kwao na kujikuta wakijiingiza kwenye mambo yasio na manufaa kwao. je watoto wasipo pewa malezi bora wataweza kuishi kwa maadili mema?
Wazazi inawapasa wawe makini na kufuatilia mienendo wa watoto wao. Inabidi wazazi wajijengee utaratibu wa kuwaweka chini watoto wao na kuvunja ukimwa na kutilia mkazo yale watoto wanayo fundishwa shuleni hususani elmu juu ya UKIMWI.
 mfano jinsi ya kuepukana na tabia hatarishi kama kuvuta bangi, sigara, kunywa pombe,kuangalia filamu za ngono na kujihusisha na vitendo vya zinaa kama walimu wao wanavyo wafundisha wakiwa mashuleni.
Ukali wa wazazi kwa watoto haujengi bali unatengeneza uadui bainia yao na inakuwa vigumu watoto wao kuwa wazi mbele yao na kuwaeleza mambo tofauti tofauti wanayo kutana nayo mitaani au mshuleni.  Wazazi wakitengeneza utamaduni mzuri wa urafiki na watoto wao, itawasidia kujua mienendo ya watoto wao na kujua wapi pakurekebisha na kutilia mkazo ili kuhakikisha watoto wao wanakuwa salama wakati wote.
Watoto hupendelea kuangalia tv, na baadhi yao hupendelea kuingia kwenye mitandao hasa  watoto wa mjini. Hupendelea kangalia mambo mbali mbali kama kuangalia miziki, filamu  pamoja na picha za wasanii na mambo mengine.
Ingawaje nyumbani wazazi wana weza kuhakikisha watoto wana angalia au kutafuta mambo yanayo wafaa kwenye mitandao lakini huduma iyo hutolewa mitaani kwa malipo kiasi  na  baadhi ya watoto hutumia mwanya huo kuangalia mambo yasiyo faa mfano picha za utupu. 
Ukiachana na ilo, kuna majumba ya sinema ambayo huonesha filamu za ngono na watoto wakiwepo bila kujali ili mradi wamelipia kiingilio.           Tabia hizi ni hatarishi na zina weza kuwashawishi watoto kujihusisha na zinaa na watoto wenzao au hata watu wazima. Hivyo basi wanatengeneza nafasi ya wao kupata  maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kuna vipindi vizuri sana kwenye tv vinavyo wafaa watoto. vipndi vya  burudisha kama vile michezo katuni na vingine vya kuwaelimisha kwa kutanua uelewa wao juu ya maswala mbali mbali katika jamii ikiwemo pia vipindi vinvavyo toa elimu juu ya ugonjwa wa ukimwi.
Wazazi ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wao  wanaangalia vipindi vinavyo wafaa pia matumizi mazuri ya mitandao mda wote. Mfanya kazi wa ndani sio rahisi kumsimamia mototo kwenye jambo hili kutokana na kuwa na shunguli nyingi za kufanya na wengine kuwa na uelewa mdogo kwani baadhi yao unaweza ukawakuta wana tazama picha zisizo faa wakiwa pamoja na watoto bila kujali.
Pia kwa upande mwingine wazazi wana paswa kuwajengea watoto wao msingi mzuri wa imani wakiwa bado wadogo ili iwasaidie waweze kuishi katika msingi huo mpaka watakapo kuwa wakubwa na hivyo basi kuepukana na tabia zinazo kinzana na mafundisho ya dini zao kama vile kuzini kabla ya ndoa au nnje ya ndoa.
Pengine inawawia vigumu baadhi ya wazazi kuwasimamia watoto wao kwenda kwenye mafundisho ya dini kutokana na kwanza wao wenyewe sio waudhuriaji wazuri wa ibada na shughuli mbali mbali za kidini.
Kiujumla mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi kwa watoto ni jukumu la jamii nzima. Watoto wenyewe, wazazi pamoja na walimu. Ushirikiano wao ndio utawezesha kuwasaidia watoto kujiandaa na mupambano dhidi ya changamoto mbali mbali zinazo wakabili watoto hususani  utandawazi.
Wahenga walisema “samaki mkunje angali mbichi” nivigumu sana kumbalilisha mtu tabia akiwa amesha kuwa mtu mzima ndo maana elimu ya ukimwi inatolewa sana kwa vijana pamoja na watu wazima lakini maambukizi yamekuwa yakiongezeka sana hasa kwa watu walio kwenye ndoa.
Kwa hali hiyo basi wazazi kushirikiana na walimu wana jukumu kubwa sana kuhakikisha wana waandaa watoto vizuri ili waweze kuepukana na tabia hatarishi zinazo weza kuwapelekea watoto wao kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Arnold musaroche
Tumaini University
0718636856








0 comments:

Post a Comment