Pages

Labels

Tuesday, June 19, 2012

PROFESA .GEORGE SAITOTI ALIYEKUWA WAZIRI WA USALAMA WA NDANI NCHINI KENYA


Aliyekuwa waziri wa  Usalama wa Ndani wa Kenya George Saitoti alifariki dunia hivi karibuni katika ajali ya helikopta iliyoanguka katika eneo la Ngong katika viunga vya jiji la Nairobi. Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya na walinzi wao pia walifariki dunia katika ajali hiyo.

Waziri Mkuu wa Kenya Bwana Raila Odinga ambaye alitembelea eneo la ajali hiyo aliwaambia waandishi habari kwamba hadi sasa sababu ya ajali hiyo bado haijajulikana. Odinga ametoa amri ya kufanyika uchunguzi kujua chanzo cha ajali hiyo.

Prf. Saitoti alikuwa mpinzani mkubwa wa kundi lenye misimamo mikali la al Shabaab la Somalia. Daima alikuwa akisisitiza kwamba serikali ya Kenya italiangamiza kabisa kundi hilo linalohatarisha usalama na amani huko Somalia na Kenya. Kwa msingi huo baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kuwa huenda kifo cha Prf. Saitoti si ajali ya kawaida na kwamba kuna uwezekano kundi la al Shabaab lina mkono katika tukio hilo. Dhana hii inatiwa nguvu zaidi na taarifa iliyotolewa na kundi la al Shabaab ambalo limefurahia kifo cha Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya.

Prf. Goerge Saitoti aliyekuwa na umri wa miaka 66 alikuwa mwanasiasa mkongwe na alikuwa mgombea urais katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika Machi mwakani. Japokuwa kampeni za uchaguzi wa rais bado hajianza rasmi nchini Kenya lakini tayari wagombea katika zoezi hilo wameanza kujinadi.

Nchini Kenya kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika chini ya jangwa la Sahara, kampeni za uchaguzi hufanyika kwa misingi ya kikabila. Sera hizi za kikabila pia hutawala shughuli nyingi za kisiasa na mahusiano na vyama na makundi mbalimbali.

Prf. Saitoti ana mfungamano mkubwa na makabila mawili ya Masaai na Kikuyu na aliheshimika nchini Kenya kama mwanasiasa mkongwe. Alinza shughuili za kisiasa yapata miongo miwili iliyopita akiwa mbunge. Baada ya hapo alihudumu serikalini kwa kipindi cha miaka 13 akiwa makamu wa rais wa Kenya. Baada ya kuchukua madaraka Mwai Kibaki hapo mwaka 2008, Saitoti alikuwa mshauri mkuu na wa kutegemewa wa kiongozi huyo na kwa msingi huo kifo chake kimeacha pengo kubwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Kenya.


 ANNA MADEU
TUMAINI UNIVERSITY

0 comments:

Post a Comment