Pages

Labels

Tuesday, July 30, 2013

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF) WAZINDUA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI

Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bi.Constantina Martin (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Mpango Mpya wa uchangiaji wa hiari mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi wasio wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii fursa ya kujiunga na mfuko huo, kushoto ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, mipango na Utafiti Bw. Gabriel Silayo.
Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mipango na Utafiti kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Gabriel Silayo (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo yaliyofikiwa na mfuko huo tangu kuanzishwa kwake kulia ni Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko huo Bi.Constantina Martin.
PICHA NA FRANK MVUNGI

Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi kutoka  (PSPF) Bi.Constantina Martin amesema Mpango huu wa hiari ni mahsusi kwa ajili ya kuwapatia huduma ya hifadhi ya jamii wale wote ambao awali kutokana na matakwa ya kisheria hawakuweza kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.  Vile vile mpango huu ni fursa nzuri ya kujiwekea akiba ya ziada wanachama ambao tayari wamo katika Mifuko mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii.
Ameongeza kuwa, uanachama katika mpango huu uko wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.  Kiasi cha mchango kwa mwezi ni shilingi 10,000/= kiwango ambacho wengi wanaweza kukimudu kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu. Michango inaweza kuwasilishwa kwa siku, wiki, mwezi na hata kwa msimu kutegemeana na upatikanaji wa kipato cha ziada. Michango hii huwekewa faida kila baada ya miezi sita.
Michango inaweza kuwasilishwa kupitia akaunti ya benki, au kupitia Wakala wa malipo wa M-Pesa, Tigo-Pesa na Airtel money. Mwanachama atajaza fomu na kupewa kitambulisho na nambari ya uanachama.
Mafao yatolewayo katika mpango huu wa hiari ni kama Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali,  Fao la Uzeeni,Fao la Ugonjwa na Fao la Kifo.
Pia mwanachama anapolazimika kuchukua michango yake yote na faida kutokana na sababu zozote zile, anaweza tena kuanza kuchangia upya bila masharti yoyote.

0 comments:

Post a Comment