Pages

Labels

Monday, July 29, 2013

MFUMO MPYA WA KULIPA ADA ZA MWAKA ZA MAGARI KWA NJIA YA MTANDAO

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Richard Kayombo (kulia) akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mamlaka hiyo Bw. Ramadhani Sengali.


Kaimu Meneja Magari kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Julius Mchihiyo (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.Meneja wa Mradi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Ramadhani Sengali akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua jinsi gani mfumo huo utaleta tija hasa katika ukususanyaji wa kodi, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari, kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka hiyo Bw. Richard Kayombo.
{PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO}

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Imeeleza kuwa Kuanzia mwezi Agosti 2013 malipo yote ya ada za mwaka za magari (annual road license) yatafanywa kwa njia ya mtandao kwa maana ya kutumia simu za kiganjani, benki na wakala wa Maxmalipo.
Hii inatokana na maboresho ya mifumo ya kielektroniki ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kuyafanya ikiwa ni juhudi za kutoa huduma bora kwa walipakodi na kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanayokusanywa na yanawasilishwa kwa wakati kwenye mfuko mkuu wa Serikali, Benki Kuu.

Mfumo huu utatumika kulipa ada za mwaka za magari ambapo mlipakodi anaweza kupata taarifa ya kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa.

Utaratibu wa kutumia mtandao kulipa ada za magari:

  1. Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za  gari mfano KADIRIA T171AUC kwenda namba 15341.  
  2. Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
  3. Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, MPESA, AIRTELMONEY au wakala wa MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.
Kuchukua cheti: (sticker ya gari): nenda katika ofisi yoyote ya TRA ukiwa na namba ya kumbukumbu uliyoitumia kufanya malipo


0 comments:

Post a Comment