Pages

Labels

Saturday, July 13, 2013

CHEKI PICHA ZA WISEMAN ALIVYO LAKIWA NA WANANCHI

Wiseman Luvanda, aliye vaa jezi ya Taifa Star nakushikilia bendera.


Wiseman Luvanda kijana aliye funga safari kutoka mbeya mpaka jijini Dar es Salaam kwa ajili yakuja kuishangilia timu yake ya Taifa, Taifa Star itakayo cheza na Uganda leo jioni amefika salama salimini nakulakiwa na mamia.

 Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 alianza safari  july 10 alifika morogoro july 11 nakuwasili jijini leo majira ya asubuhi na mapema.

Changamoto alizo kutana nazo ni pamoja na kuchoka sana akiwa njiani,  kuumwa miguu kwenye viungio (joints) lakini pia kuombwa pesa njiani nawatu walio fikiri ana fadhiliwa.

Baadha ya wakazi wa morogoro kijiji cha centrol kingolwira akiwemo bwana Omar Salum amesema kijana huyo amefanya jambo la kizalendo nakuongeza ni changamoto kwa vijana wengine.

 Lakini pia walionesha hofu ya usalama wa kijana huyo kwani hakuwa na ulinzi wowote na alipita maeneo hatarishi.

by Agnes Mbonimpa

1 comment: