Pages

Labels

Wednesday, July 10, 2013
Wizara ya viwanda na biashara imewataka wafanya biashara inchini kutumia vyema fursa walizo nazo kwa kufanya biashara na nchi wahisana wa Afrika mashariki, kwani wao kama wizara wamejitaidi kujenga mahusiano mazuri na inchi za ukanda huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mapema leo hafisa habari na mawasiliano wa wizara hiyo Bw. Nikodemas Mushi amewataka wafanya biashara wafike wizarani ili wapata maelekezo jinsi gani wanaweza kufanya biashara kwenye soko la Afrika mashariki,  pamoja na SADEC.

“wafanya biashara wanapaswa kuuza vitu vyenye ubora unao  hitajika pamoja na ujazo stahiki ili waweze kupata soko kwenye jumuiya ya Afrika mashariki, hivyo basi ningezitaka kampuni na taasisi kuwekeza katika utengenezaji wa vifungashio  ili kuwasidia wajasiria mali wadogo wadogo kuepukana na kutumia vifungashio visivyo na ubora” alisema 

Mushi pia aliwata wafanya biashara kuzingatia ujazo ulio sahihi nakuacha kujaza lumbesa.

Hata ivyo hafisa huyo wa habari amesema pamoja na kufanya operesheni mbali mbali za kushtukiza ili kubaini bidhaa ambazo hazija thibitiswa na mamlaka ya viwango (TBS)  amewataka  pia wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo ili kubaini bidhaa zinazo ingizwa inchini kinyemela kwani nyingi zinakua hazina ubora. 

Arnold Musaroche 
0656 606095

0 comments:

Post a Comment